22 Julai 2024 - 08:43
Maarifa yote katika mambo manne

Mtu ambaye hajui jibu la maswali haya, bila shaka hajui chochote.

Imam al-Sadiq (a) anasema:

وَجَدْتُ عِلْمَ اَلنَّاسِ كُلَّهُ فِي أَرْبَعٍ

Nimepata maarifa yote ya watu katika mambo manne.

أَوَّلُهَا أَنْ تَعْرِفَ رَبَّكَ

Kwanza, ujue Mungu wako. muumba wako ni nani?

وَ اَلثَّانِي أَنْ تَعْرِفَ مَا صَنَعَ بِكَ

Na pili ni kujua alichokufanyia. Alikuumbaje? Ni vitu gani ameweka ndani yako?

وَ اَلثَّالِثُ أَنْ تَعْرِفَ مَا أَرَادَ مِنْكَ

Na tatu, ni lazima ujue Mungu anataka nini kutoka kwako.

.وَ اَلرَّابِعُ أَنْ تَعْرِفَ مَا يُخْرِجُكَ مِنْ دِينِكَ

Na ya nne ni kujua nini kinakufanya uiache dini yako.

———————————–

Na kulingna na neno la Imam al- Sadiq (a) inapaswa kusemwa kwamba mtu ambaye hajui jibu la maswali haya, bila shaka hajui chochote.

Chanzo: alanwaralmunirah